Tusome Mathayo 5:21-22
Msatari wa 22 unasema jehanamu ya moto. Haya ni maneno aliyoyasema Yesu Kristo mwenyewe yakuwa jehanamu ya moto ipo. Hatakama huamini, haitabadilisha.
Kwanini jehanamu ya moto?
Hii ni sehemu ambayo Mungu ameiandaa kwa ajili ya shetani na malaika zake. Ni sehemu ambayo ilikusudiwa kwa ajili ya watenda maovu ambao wako kinyume na Mungu mwenyenzi. Na ndiyo maana pia kuna wanadamu ambao nao wataenda huko wale ambao hawamwabudu Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo.
Je unajitayarishaje kwa ajili ya ulimwengu ujao?
Najua unajitayarisha kwa habari ya maisha yako ya hapa duniani kama kujenga nyumba kwa ajili ya familia, kupata elimu mbalimbali, kuishi vizuri na watu nk. Lakini je unajitayarisha pia kwa habari ya maisha yako ya baada ya kifo? Je unajua ukifa utaenda wapi?
Ni watu wengi sana wanaokufa kila dakika. Walio wengi hawajui ni wapi wanakwenda, wanajikuta tayari wapo kwenye maisha mengine. Je ni wangapi unaowajua walikufa wakiwa dhambini? Hawajampa Yesu Kristo maisha yao? Hivi unafikiri mtu huyo ataenda wapi bila Yesu?
Tuangalie Luka 16 kwa habari ya yule tajiri na Lazaro. Yule tajiri alipokufa, alijikuta yuko Jehanamu ya moto. Na akatamani kurudi duniani kuwaambia watu wa nyumbani kwake kuwa wasiende huko aliko. Hapa tunaona tajiri huyu ni kama anatuambia tujitayarishe hapa duniani tusisubiri kujionea hukohuko tukifika baada ya maisha haya.
Mpendwa jiandae! Tumeambiwa katika maandiko matakatifu yakuwa baada ya kifo ni hukumu. Yaani hukumu ya jehanamu ya moto au raha ya mbinguni katika Kristo Yesu.
Tunapaswa kujiandaa hapahapa duniani. Safari yako ya umilele ilishaanza toka pale ulipozaliwa. Wewe ni roho, na hapa duniani unaishi ndani ya mwili. Mwili huu ukifa utazikwa lakini wewe ambaye ni roho utaendelea kuishi na kupewa mwili mpya kutokana na sehemu utakayoelekea.
Uchaguzi ni wako mpendwa wangu. Embu kaa na utafakari mahali dunia na fahari yake yote itakapokupeleka. Mchague Yesu leo awe ndiyo kimbilio lako na maisha yako. Mwache Yesu ayatawale maisha yako sasa ili uweze kuongozwa nae kuishi vizuri hapa duniani na baadae kwenye uzima wa milele ujao.
Jua kwamba njia ya kwenda jehanamu ya moto ni pana na ni rahisi sana kuiendea. Njia ya mbinguni kwa Mungu ni nyembamba na wanaoiendea njia hii kamwe hawawezi kufanana na wale wa njia pana. Kwasababu hekima za hizi sehemu mbili ni tofauti. Njia pana inaongozwa na shetani wakati njia nyembamba inaongozwa na Roho Mtakatifu.
Haijalishi kuwa wewe ni mtumishi wa Mungu kama padri, mchungaji au mwamini. Kama hujajiweka tayari na kuiendea njia nyembamba, utajikuta uko njia pana tu itakayokupeleka jehanamu ya moto. Kuwa macho!
Jehanamu ya moto ipo. Nakusihi usiende huko. Hauhitaji kwenda huko. Mpokee Yesu leo upate kubadilisha maisha yako na kumuishia yeye.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
-
Zaburi 107:19-20 inasema “Wakamlilia Bwana katika shida zao. Akawaponya na shida zao.Hulituma neno lake huwaponya. Huwatoa katika maang...
-
Msongo wa mawazo yaani stress hutokea pale ambapo mwili unapotoa homoni za kuweza kupigana na hiyo hali ya msongo wa mawazo. Hiyo hali ikiwa...
-
Luka 12: 32-34 "Msiogope enyi kundi dogo, maana Baba yenu amependa kuwapeni ufalme. Uzeni mali yenu mkawape maskini hizo fedha. Jifa...
Hi karibuni tuchangie ili kuweza kujifunza zaidi
ReplyDeleteAmen. Ubarikiwe sana Madam
ReplyDeleteAmen asante Eagle
ReplyDeleteHakika tunapaswa kujiandaa
ReplyDeleteHakika tunapaswa kujiandaa
ReplyDeleteHakika tunapaswa kujiandaa
ReplyDelete