Monday, 20 March 2017

Ukame Umekwisha

Mpendwa msomaji wangu,
Ili kuweza kupenyeza katika ukweli wa kuishi kiuhalisia wa maisha ya kiroho (supernatural living) unahitaji uwe kama mtu aliye "mpumbavu" hivi.
1Wakorintho 1:27 inasema "Bali Mungu alivichagua vitu vipumbavu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye hekima; na Mungu alivichaguwa vitu dhaifu vya ulimwengu ili aviaibishe vitu vyenye nguvu."

Upumbavu hapa haina maana ya ujinga au asiye na akili bali inaongelea wale ambao wanajua wanahitaji huruma na msaada wa Mungu kwasababu bila ya Mungu hawawezi wao wenyewe. Wanajua wana muhitaji Bwana Yesu ili kuweza kuwasaidia kuishi yale maisha ambayo wanayatamani (desire).

Neno la Mungu liko kwa ajili ya kuleta imani moyoni na si kuleta mantiki akilini. Angalia 1 Wakorintho 1:22-23 inasema " Kwa maana Wayahudi wanaomba ishara na Wagiriki wanatafuta hekima. Lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyetundikwa mtini, kwa Wayahudi ni sababu ya kujikwaa lakini kwa mataifa ni upumbavu"

Mashindano baina ya akili (intellect) au kujisikia(feelings) na moyo (heart) ambamo imani hukaa inaweza kuonekana pale ambapo watu wanaambiwa wamtolee Mungu fungu la kumi na sadaka mbalimbali. Kama akili yako haijageuzwa na Roho Mtakatifu, basi utashi wa kibinadamu hutawala na mtu huishia kufuata hisia zake za kutokutoa. Mtu wa namna hii anakuwa ni mtu wa Ufalme wa Mungu lakini anaishi chini ya utawala wa dhambi na laana ya dunia.

Fungu la kumi na sadaka nyinginezo ni ahadi ambazo hazikwepeki kwa mtu wa ufalme wa Mungu kuzifanyia kazi kama atataka kupata mpenyo wa kifedha na maisha bora kwa ujumla wa kimwili, kinafsi na kiroho. Namna ambayo Mungu anatupa mahitaji yetu ni kwa kupitia mbegu tunazozitoa.

Ngoja nikupe mfano wa kitu halisi kilichonitokea mimi mwenyewe kwa habari ya kutoa fungu la kumi.

Kama familia kwa wazazi wangu tulikuwa tunadaiwa na benki moja bilioni 2. Sasa ikafika wakati ni lazima tuuze nyumba iliyokuwa na dhamana kwa ajili ya kulipa benki. Tukatafuta wateja kwa muda mrefu sana kama kwa miaka miwili hivi hatukuweza kupata mtu wa kuweza kuinunua. Sasa nikawa najifunza mambo mengi ya namna ya kutoka kimaisha na kuweza kupata ninachohita ji kibiblia. Nikaweza kujifunza pia kwa habari ya utoaji mbalimbali kama neno la Mungu linavyoagiza. Nikawa ninaanza kutoa fungu la kumi kwa hela ndogo nazopata. Baada ya muda nikawa ninafuatilia mafao yangu ambapo nilikuwa nimeacha kuajiriwa na kuingia kujiajiri. Nilivyopokea tu yale mafao nikakumbuka natakiwa nitoe fungu la kumi. Ingawa hela ilikuwa kubwa ya kutoa maana ili kuwa kwenye milioni kadhaa hivi nikajitia moyo na kusema hapa ndipo imani yangu itakapopimwa.
Nikaamua kuitoa na nikaiombea iweze kufungua nyumba yetu iweze kuuzika.
Kesho yake baada ya kutoa hiyo fedha, kuna dalali ambaye hatukuwa tunafanya nae kazi wala hatumjui akaja asubuhi na mapema na kusema nasikia mnapauza hapa na nimekuja na mteja. Kwakweli waliponipigia simu na kuniambia niliona kama ni wale wale tu maana tulishazoea watu kuja na kuyeyuka. Nahapo watu wa nyumbani kwangu hawakujua kama kuna hela nimetoa kama sadaka tena nyingi maana wasinge nielewa.

Lakini yule mteja alikuwa serious na akasema twende mkanitambulishe benki kuwa mimi ndiyo nitanunua. Maana hapo benki walikuwa wametupa wiki mbili tu wao watakuja kuinadi. Basi tukampeleka na akajicomit na kuanza kutoa hiyo hela. Na alipo maliza kulilipa hilo deni akatupatia na sisi hela nyingi tu kwa ajili ya kuendelea na maisha. Kwakweli Mungu ni mkubwa kwasababu nilimuona Mungu amefanya kama alivyosema katika neno lake kwamba hatakawia tusipovunjika mioyo.

Sasa embu tuone tulichojifunza kutokana na ushuhuda huu;
Kwanza, huwezi kupata jaribu lolote kubwa ambalo huwezi kulivuka. 1 Wakorintho 10:13. Katikati ya hitaji nilikubali kufanya kitu ambacho kilimgusa Bwana na mbegu hiyo ikafungua madirisha na kuondoa ukame uliokuwepo.

Pili, Gundua mbegu yako na uwe tayari kuipanada na siyo kuisevu au kuila. Kumbuka, kama ukitoa kilichoko mkononi mwako, na Bwana atatoa kilichoko mkononi mwake kwa ajili yako. Bwana anao Ulimwengu mzima mikononi mwake 1Wafalme 17.

Tatu, Unaweza ukaiamulia mbegu yako ifanye chochote unachokitaka ifanye. Mbegu yako inaweza kuwa chochote kinacho mbariki mtu mwingine.

Nne, Siyo sana ukubwa wa mbegu yenyewe bali ni imani iliyowekwa kwenye hiyo mbegu. Mavuno utakayoyapata ni makubwa mno kuliko mbegu uliyoitoa. Marko 12:43.

Tano, Hakuna janga lolote kubwa litakaloondoa hii kanuni ya kupanda na kuvuna isifanye kazi kwako kama utaizingatia. Hii kanuni itaendelea kufanya kazi na ni ya milele kama usiku na mchana. Mwanzo 8:22, Jeremia 33:19.

Kwahiyo kama utatamani kuondoka kabisa kwenye hiyo hali uliyonayo ya ukame katika maisha yako, anza kufanyia kazi maneno haya niliyokuambia uone kama maisha yako hayatabadilika na kuwa kama unavyo tamani siku zote. INAWEZEKANA!
 
 

6 comments:

  1. Hi. karibu uchangie ili kuweza kujifunza zaidi.

    ReplyDelete
  2. Ubarikiwe mtumishi wa Mungu aliye hai. ...nmejifunza mambo makubwa sana. ....

    ReplyDelete

  3. Neno la Mungu liko kwa ajili ya kuleta imani moyoni na si kuleta mantiki akilini. Angalia 1 Wakorintho 1:22-23 inasema " Kwa maana Wayahudi wanaomba ishara na Wagiriki wanatafuta hekima. Lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyetundikwa mtini, kwa Wayahudi ni sababu ya kujikwaa lakini kwa mataifa ni upumbavu"

    This is my favourite phrase Ukundi. Imearikiwa sana.. Ubarikiwe sana. Naendelea kujifunza

    ReplyDelete
  4. Asante sana Mtumishi Ukundi kwa solo hili kuu juu ya kumtolea Mungu. Nimejifunza mengi na nitajitahidi kuyatenda ili Bwana anifungulie milango pia. Ubarikiwe sana.

    ReplyDelete
  5. Asante Martin. Mungu wetu ni mwaminifu. Mara zote anasubiri ufanye neno lake nae akutendee aliyokuahidi. Ubarikiwe

    ReplyDelete
  6. Asante EagleEye. Karibu tuendelee kujifunza

    ReplyDelete