Habari za leo mpendwa msomaji wangu.
Karibu kwenye somo hili la namna ya kuishinda dhambi.
Watu
wengi wanajiuliza ni kwa namna gani mtu anaweza kuishinda dhambi akiwa
hapa duniani. Embu tuangalie Waefeso 2:1-10 inasema:
"Ninyi mlikuwa mmekufa kwa sababu ya makosa na dhambi zenu. Wakati
ule mliishi kufuatana na mtindo mbaya wa ulimwengu huu, mkawa mnamtii
mtawala wa pepo wenye nguvu wa anga, pepo ambao huwatawala sasa watu
wasiomtii Mungu. Na
hata sisi sote tulikuwa kama wao; tuliishi kufuatana na tamaa zetu za
kidunia na kufanya tu mambo yale yaliyoipendeza miili na akili zetu.
Kidunia, sisi kama vile pia wao, tulistahili ghadhabu ya Mungu. Lakini Mungu ni mwenye huruma nyingi. Alitupenda kwa mapendo yasiyopimika, hata, ingawa tulikuwa tumekufa kwa sababu ya dhambi, alitufanya hai pamoja na Kristo. Kwa neema ya Mungu ninyi mmeokolewa. Kwa kuungana na Kristo Yesu, Mungu alitufufua pamoja naye, tukatawale pamoja naye mbinguni. Ndivyo
alivyopenda kuonyesha kwa watu wa nyakati za baadaye, ukuu wa neema
yake aliyotujalia kwa ukarimu katika kuungana kwetu na Kristo Yesu."
Hapa
tunaona kuwa kwa kitendo cha kuungana na Yesu Kristo yaani kumpokea
Yesu katika maisha yako na moyo wako, unaweza kupata neema kwa Mungu ya
kukufanya hai tena pamoja na Kristo wakati ulikuwa umekufa kwasababu ya dhambi zako. Kwahiyo sasa umefufuliwa na Yesu Kristo ili ukatawale nae mbinguni.
Cha
kujiuliza hapa nikuwa unawezaje kutawala na Yesu mbinguni wakati
unaishi bado katika maisha ya dhambi? Neno la Mungu linasema katika Ufunuo 21:27 hakuna kinyonge kitakachoingia mbinguni na kuna sehemu nyingine inasema Mungu hupendezwa na watakatifu walioko duniani. Je unataka kuwa mtakatifu wewe hapa hapa duniani? Je ni kwa namna gani unaweza kufanikiwa kuacha dhambi.
Tunajua
ya kuwa Mungu wetu ni mtakatifu, nae hukaa mahali patakatifu yaani
ndani ya moyo wako. Ili uweze kushirikiana na huyu Mungu mtakatifu,
inakubidi na wewe uwe mtakatifu na kuishi maisha matakatifu.
Unaweza
kuwa mtakatifu kama utaamua. Kumbe tunaona UAMUZI wako ni kitu muhimu
sana katika wewe kuweza kuishi maisha matakatifu au la.
Je ni kwa namna gani?
Ili
kuweza kuacha kabisa dhambi unatakiwa uamue kufanya hivyo. Amua toka
ndani ya moyo wako kuwa dhambi ni uasi kwa Mungu na kuwa inamchukiza
Mungu. Pia utambue kuwa kwa kufanya dhambi unaweza usipate muda wa
kutubu na ikakupelekea kwenda motoni. Ukiisha kukaa na kutafakari ndani
yako kwa habari ya madhara ya dhambi yoyote ile iwe ni kubwa au ndogo,
ndipo utakapopata majibu ya namna gani uichukulie dhambi.
Neno la Mungu linatuambia tuchague kumpenda Mungu na kuachana na dhambi ili tupate uzima wa milele. Sema hapana
kwa dhambi yoyote hata kama inakufurahisha kwa namna gani. Fikiria kuwa
hiyo raha au starehe unayoipata sasa hivi kwa kuifanya hiyo dhambi
itageuka uchungu wakati ujao na utajutia.
Ni kwa jinsi gani unaweza ukawa na uamuzi unaofaa?
Ni
kwa kuanza kuwaza mwisho wako (future) unaotaka uweje. Ukishakuwa na
picha ya mwisho wako au future yako, ni rahisi kuweza kupangua vitu
ambavyo vinaweza kukwamisha katika kuufikilia huo mwisho mwema
unaoutarajia.
Mfano,
unataka kuingia mbinguni na kumuona Mungu mwisho wa maisha yako. Na
unakutana na mtu anakuambia nakupenda twende tukazini japo kidogo tu.
Kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya ni kuufikiria au kujikumbusha ule
mwisho wako ni nini halafu rudisha mawazo yako katika hicho kitu ambacho
hata wewe mwenyewe unakitaka kukifanya kwa saa hiyo, halafu jiulize je
kwa kufanya hiki kitendo naweza kuhatarisha maisha au kuyaendeleza
maisha. Ukishapata jibu kuwa unaweza kuhatarisha kwasababu huenda
unaweza ukafa ukiwa katikati ya hilo tendo au Yesu akarudi ukiwa
katikati ya hilo tendo.
Ukishaweza kupata
jibu la hapana sitafanya ni lazima uanze kufikiria namna ya kuondoka au
kukaa mbali na hilo jambo, au huyo mtu au hiyo sehemu nk.
Biblia inatuambia tuikimbie dhambi kama Yusuphu alivyoikimbia dhambi hii kutoka kwa yule mke wa farao.
Uzuri
ni kwamba kila wakati ukichagua kufanya uamuzi sahihi, hatimaye Roho
mtakatifu anakusaidia kuondoa tamaa ya hicho kitu ndani yako na unaanza
kuwa HURU kabisa mbali na hiyo dhambi. Na hii ni kwa watu wote wanaume
na wanawake, watoto, vijana na wazee.
Mpendwa
msomaji wangu. Ninajua kuwa hili somo si rahisi sana kama tunavyoongea,
lakini kwa msaada wa Mungu na Roho Mtakatifu tunaweza tukashinda dhambi
kabisa na kuwa huru kama vile Mungu anavyosema Watakatifu walioko
duniani ndiyo ninaopendezwa nao.
Kumbuka dhambi moja ni mlango wa kuleta dhambi nyingine.
Anza leo KUAMUA kuachana na hiyo dhambi inayokusumbua kila wakati na
kuitubia kila wakati uone utakavyokuwa huru na kuishinda kabisa. "INAWEZEKANA KUWA HURU MBALI NA DHAMBI"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
-
Zaburi 107:19-20 inasema “Wakamlilia Bwana katika shida zao. Akawaponya na shida zao.Hulituma neno lake huwaponya. Huwatoa katika maang...
-
Msongo wa mawazo yaani stress hutokea pale ambapo mwili unapotoa homoni za kuweza kupigana na hiyo hali ya msongo wa mawazo. Hiyo hali ikiwa...
-
Luka 12: 32-34 "Msiogope enyi kundi dogo, maana Baba yenu amependa kuwapeni ufalme. Uzeni mali yenu mkawape maskini hizo fedha. Jifa...
Hakika ilikushinda dhambi ni lazima uwe karibu na Mungu umsogogelee yeye na uwepo wa Mungu (uhamsho) ambapo automatic itakutenga mbali na dhambi na kukufanya uwe katika uwepo wa Mungu
ReplyDeleteits true brother
ReplyDelete