Friday, 17 March 2017
PALE ILIPO HAZINA YAKO, NDIPO ILIPO NA MOYO WAKO
Luka 12: 32-34
"Msiogope enyi kundi dogo, maana Baba yenu amependa kuwapeni ufalme. Uzeni mali yenu mkawape maskini hizo fedha. Jifanyieni mifuko isiyochakaa na kujiwekea hazina mbinguni ambako haitapungua. Huko wezi hawakaribii wala nondo hawakaribii. Pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako."
Je umewahi kujiuliza ni kwanini unapenda sana kitu Fulani au mambo fulani katika maisha? na jambo hilo unalifikiria sana usiku na mchana? Hii ni kwasababu nguvu yako yote ya hali na mali umeielekeza huko. Napia ni kwasababu unajitahidi sana kwa nguvu zako kuhakikisha hicho kitu kinakaa vizuri kama upendavyo na hii ni kwasababu hicho kitu kinathamani sana katika maisha yako.
Biblia inatuambia popote hazina yako ilipo pia moyo wako upo. Ukiona umeconcentrate sana mahali Fulani ujue kuna hazina yako.
Je wewe umeconcentrate zaidi wapi katika maisha yako? Ni upande wa Mungu au wa dunia?
Yesu anatuambia tusiogope kwa maana Baba wa Mbinguni anataka kutupa ufalme. Lakini sharti tujiwekee hazina zetu mbinguni. Kwanini alisema hivyo? Tena akasema mkaviuze mlivyonavyo.
Hii inamaana kuwa tunatakiwa kusalimisha hazina zetu zote kwa Bwana Yesu kwasababu mahali hazina ilipo na moyo huwa hapohapo.
Kama utakuwa unamtegemea Bwana Yesu katika kazi zako zote na kuamini kuwa yeye ndiye msimamizi wa kila jambo basi na moyo wako utamtafakari yeye siku zote na kumpa yeye utukufu katika kila jambo ambalo unalifanya au unalipata.
Watu wengi wanatumia hazina zao kinyume na mapenzi ya Mungu kwa kujifurahisha wenyewe na kwasababu wanatumia kwa maslahi yao, na moyo wao unakuwa hukohuko ambako fedha zao wameweka. Mfano Unamkuta mtu anabadilisha maumbule yake kwa kufanyiwa operesheni ili awe na matako au maziwa mazuri au kiuno kizuri au sura nzuri nk. Hiyo fedha ambayo ni hazina yake ameitumia kujifurahisha mwenyewe na huku akimkosoa Mungu kuwa hakumuumba vizuri hii ni dhambi inayopaswa kutubiwa na kuachwa mara moja. Mtu huyu utakuta kila wakati anajiangalia yeye mwenyewe na moyo wake uko katika kujiangalia kama amependeza au watu wanamuonaje na hii ni mfano tu wa ilipo hazina yako na moyo wako upo hapo.
Wengine ni wagonjwa, badala ya kumuangalia Kristo na kutafakari njia zake na maneno yake ya uponyaji, wao wanatumia fedha zao na nguvu zao kwenda kwa waganga na ndiko huko moyo wao unapo kuwa kwasababu wanategemea huko.
Hatakama unatumia dawa za hospitali, unatakiwa kuweka moyo wako kwa Yesu Kristo zaidi kwa kukiri maneno yake ya uponyaji.
Nakusihi ujichunguze kama ni kwa jinsi gani unatumia hazina yako . Unaitumia kwa manufaa yako binafsi au kwa utukufu wa Mungu. Kwasababu hazina na moyo ni vitu vinafuatana pamoja.
Pale hazina yako ilipo na ndipo na moyo wako unapokuwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
-
Zaburi 107:19-20 inasema “Wakamlilia Bwana katika shida zao. Akawaponya na shida zao.Hulituma neno lake huwaponya. Huwatoa katika maang...
-
Msongo wa mawazo yaani stress hutokea pale ambapo mwili unapotoa homoni za kuweza kupigana na hiyo hali ya msongo wa mawazo. Hiyo hali ikiwa...
-
Luka 12: 32-34 "Msiogope enyi kundi dogo, maana Baba yenu amependa kuwapeni ufalme. Uzeni mali yenu mkawape maskini hizo fedha. Jifa...
Hi karibuni tuchangie ili kuweza kujifunza zaidi.
ReplyDeleteAmen , it's real interesting
ReplyDeleteAsante Saul, Karibu
ReplyDelete