Warumi 8:1-2
“Sasa basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika
Kristo Yesu. Kwasababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu
imeniacha huru mbali na sheria ya dhambi na mauti.”
Hii ni kwa namna gani?
Kipindi kile cha sheria ya Musa, watu walikuwa wanaishi
kutegemea mwili na si rohoni. Mwili ni dhaifu kwa habari ya kufuata sheria za
Mungu. Hii ilitokana na laana ya dhambi iliyofanyika pale katika bustani ya
Edeni ambapo Eva alidanganywa na nyoka na kula tunda alilokatazwa na Mungu.
Walipoondolewa kutoka bustanini, utawala wote waliokuwa nao Adam na Eva uliingia
mikononi mwa shetani ambaye ni mleta laana.
Hata sheria ya Mungu iliyoletwa na Musa ilipokuja, kwasababu
ya laana, watu hawakuweza kuitimiza
sheria. Watu walibaki wakiwa wanahukumiwa kwasababu ya dhambi zao na kuishi maisha
ya kushindwa kila wakati.
Ashukuriwe Mungu mwenyenzi kumleta Yesu Kristo mwanane na
kuja kufa kwa ajili yetu na kuondoa sheria ya dhambi na mauti iliyoletwa na
shetani, na kuweka sheria ya uzima ndani ya kila atakaye muamini. Ukiamua
kumwamini Kristo Yesu, basi hakutakuwa na hukumu ya dhambi na mauti juu yako
kwasababu sheria ya roho wa uzima inakuweka huru mbali na sheria ya dhambi na
mauti. Na hii inawezekana kwasababu wewe utakuwa hauenendi tena katika mwili ambao
ni dhaifu kupokea sheria za Mungu, bali uko katika roho ambamo sheria ya Mungu
inawekwa ndani yako automatically, wala hutakuwa na haja ya kutumia nguvu
kuacha dhambi. Utajikuta tu unajua hii ni dhambi na hivyo utaachana nayo au
utakaa mbali nayo.
Mpendwa msomaji ukiona bado unatumia nguvu sana kuacha
dhambi na kwa muda mrefu, nakusihi ujichunguze kwa habari ya wokovu wako
kwasababu hutakiwi kuishi na tamaa za mwili wakati unatakiwa kutawaliwa na Roho
Mtakatifu ili akuweke huru mbali na dhambi na mauti.
No comments:
Post a Comment