Mtu atashiba mema kwa matunda ya kinywa chake. Mithali 12:14
Chochote mtu atakachokuwa anatamka katika kinywa chake ndicho atakifanya kiwe kama alivyotamka. Ni vema kutamka mema kwako na kwa wengine. Hata siku moja usikubali kutamka neno ovu ama linaloonyesha udhaifu fulani katika maisha yako na ya wengine. Kwasababu, kwa kutamka maneno unayapa uwezo wa kufuatiliwa na nguvu iliyoko nyuma ya hayo maneneo na kuleta sawasawa na hiyo nguvu ilivyotafsiriwa na ubongo wako.
Anza leo kufuta maneno yote hasi uliyowahi kutamka kwako mwenyewe na kwa wengine. Anza leo kutamka maneno chanya yenye kuleta amani na ushindi juu ya maisha yako na ya wengine pia.
Kwa mfano: Usiseme "Sitaki kufeli"
Sema " Nataka kufaulu"
Jua ya kuwa, ukisema sitaki kufeli, kuna nguvu ambayo inaambatana na hilo neno ambalo ni nguvu hasi yenye kuleta hofu. Hofu ya kufeli. Kwahiyo hatakama hutaki kufeli, maadamu umeshataja kufeli, hiyo nguvu huambatana na neno na kukupa hilo hitaji la kufeli.
Ukisema nataka kufaulu, vivo hivyo kuna nguvu nyuma ya hilo neno. Nguvu chanya ya ushindi ambayo itakupelekea kushinda.
Kumbe maneno nayo yana nguvu nyuma yake ya kupelekea ubongo (subconcious) ifanye kama inavyojisikia kutokana na nguvu iletayo hisia (emotions) zilizojengeka wakati wa kutamka hayo maneno.
Hivyo basi ili kuweza kupata hitaji lako, unatakiwa
- Ulifikirie (think about it)
- Ulitamke kwa mtazamo chanya (speak out loud)
- Weka hisia (emotions) hapa ni hali utakavyojisikia kama vile umeshalipata hitaji lako.
- Lipokee (receive)
- Litakuwa lako (will be yours)